MAREKANI-TRUMP-HAKI

Jaji Kavanaugh akabiliwa na mashtaka mapya

Brett Kavanaugh ambaye Rais Donald Trump alikua anatarajia kumteua kuwa mkuu wa Mahakama Kuu nchini Marekani akiwa mbele ya Kamati ya sheria ya Bunge la Senate, Septemba 4, 2018.
Brett Kavanaugh ambaye Rais Donald Trump alikua anatarajia kumteua kuwa mkuu wa Mahakama Kuu nchini Marekani akiwa mbele ya Kamati ya sheria ya Bunge la Senate, Septemba 4, 2018. REUTERS/Joshua Roberts

Uteuzi wa Brett Kavanaugh kwenye Mahakama Kuu ya Marekani umeingiliwa na mashtaka mapya ya unyanyasaji wa kijinsia. Kesi hii ni ya toka ujana wake na kuonekana kuwa ni pigo jingine kwa Donald Trump katika kumteua kwenye nafasi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Julie Swetnick, mfanyakazi wa serikali, amemshtumu Bw Kavanaugh kuwa katika kundi la wavulana katika "miaka ya 80" ambao walikuwa wakijaribu kuwanyeshwa wasichana pombe haramu na madawa ya kulevya ili kuwatumia kimapenzi.

Katika taarifa iliyowasilishwa kwa Bunge la Seneti, Bi Swetnick, mwenye umri wa miaka 50, pia amedai kuwa mwenyewe alibakwa na kundi la watu wakati wa Sikukuu ambapo Brett Kavanaugh "alikuwepo" katika miaka ya 1982.

"Simjui mtu huyo na hayo anayozungumzia hayajawahi kutokea," amekanusha Brett Kavanaugh, mwenye umri wa miaka 53, huku akishtumu katika taarifa fupi shambulizi "baya" kutoka "ngazi ya nne".

Rais Trump, anayemuunga mkono hadi sasa, alimuunga mkono kidogo kuliko kabla wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko New York.

Kwa upande mmoja, alikanusha "kashfa kubwa" iiliyotengenezwa na chama cha Democratic ili kutengua uthibitisho wa mgombea wake na kumsifu "muungwana", "mtaalamu wa ajabu".

Kwa upande mwingine, amehakikisha kuwa anaweza "kubadili msimamo wake" baada ya kusikia ushahidi kutoka kwa mlalamikaji wa kwanza, Christine Blasey Ford, mwenye umri wa miaka 51, ambaye anatarajiwa kusikilizwa Alhamisi wiki hii na tume ya Bunge la Seneti.