Chama cha Democratic charejesha udhibiti wa bunge la Wawakilishi Marekani
Imechapishwa:
Chama cha Democratic kimepata ushindi katika bunge la Wawakilishi huku, huku kile cha Republican kikipata ushindi katika Bunge la Senate, ushindi ambao unamaanisha kuwa Rais Donald Trump ataendelea kupata uungwaji mkono wa juu kwenye bunge hilo.
Ushindi wa Democrats katika bunge la Congress, ina maanisha kuwa, watakuwa na uwezo sasa wa kukwamisha ajenda ya rais Donald Trump, lakini Trump anasema ushindi wa chama chake katika bunge la Senate ni mafanikio.
Nancy Pelosi, kiongozi wa chama cha Democratic bungeni anatarajwia kuwa spika mpya.
Kwa matokeo haya ni wazi kuwa Rais Donald Trump atapata wakati mgumu wakati atakapoomba kuteuliwa tena na chama chake katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Kabla ya Uchaguzi huu, chama cha Republican kilikuwa kinadhibiti mabunge yote mawili.