Mjadala wa Wiki

Marekani: Democratics washinda bunge la wawakilishi, Republican watawala Senate

Imechapishwa:

Chama cha Republican cha rais Donald Trump, kimepata ushindi katika bunge la Senate huku kile cha Denocratic, kikirejesha udhibiti wa bunge la wawakilishi, baada ya matokeo ya Uchaguzi wa Wabunge, Maseneta na Magavana, uliofanyika siku ya Jumanne. Matokeo haya yanamaanisha nini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Kujadili hili, ni Abdulkarim Atiki, mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa mjini Arusha nchini Tanzania na Dokta Brian Wanyama, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kibabii mjini Bungoma nchini Kenya.

Wafausi wa Democrats wakisherehekea ushindi wa wabunge Novemba 7 2018
Wafausi wa Democrats wakisherehekea ushindi wa wabunge Novemba 7 2018 REUTERS/Leah Millis