California yaendelea kukumbwa na moto mkubwa, 59 wapoteza maisha
Imechapishwa:
Moto unaoendelea katika Jimbo la California tayari umesababisha vifo vya watu wasiopungu 59 kulingana na ripoti mpya. Mamlaka zinaendelea na juhudi za kuwapata watu 130 ambao bado hawajapatikana.
"Miili nane ya watu waliofariki dunia ilipatikana" jana Jumatatu huko Paradiso, mji mdogo wa kaskazini mwa California uliokumbwa na mkasa huo wa moto Novemba 8, na kufisha jumla ya idadi ya vifo 56, " Mkuu wa Kaunti ya Butte, Kory Honea, amesema.
"Tumepata miili 47 na tumeanza mchakato wa kutambua watu hao, lakini tunasubiri uthibitisho wa vipimo vya damu (DNA)," Kory Honea ameongeza katika mkutano na waandishi wa habari, akitangaza kuwa vifaa vya hali ya juu vya vipimo vya damu vimeanza kuwasili kwenye kwenye eneo kunakohifadhiwa miili hiyo.
"Kuanzia kesho, yeyote aliyempoteza ndugu yake kufuatia mkasa huyo wa moto anaweza kuja na kutupa sampuli ya DNA," amesema Mkuu wa Kaunti ya Butte, ambaye anataka kuweka kipaumbele kwa kutafuta waathirika wa "Camp Fire" , moto mbaya zaidi katika historia ya Jimbo hili la magharibi mwa Marekani.