MAREKANI-CALIFORNIA-MAJANGA ya ASILI

California: Zoezi la kutambua miili ya waathirika wa mkasa wa moto laanza

Maafisa wakiendelea na shughuli ya kutafuta miili ya watu waliofariki katika mkasa wa moto mkubwa california.
Maafisa wakiendelea na shughuli ya kutafuta miili ya watu waliofariki katika mkasa wa moto mkubwa california. © AFP

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia Jumamosi kuzuru Jimbo la California, linalokumbwa kwa wiki kadhaa na mkasa wa moto mkubwa ambao umeua watu zaidi ya 62. Zoezi la kutambua baadhi ya miili kwa njia ya vipimo vya damu (DNA) limeanza.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa imeingia siku ya nane leo Ijumaa, moto huo ukiendelea kuathiri baadhi ya maeneo ya California, mamlaka zinaendelea kutafuta waathirika wa "Camp Fire", moto mkubwa uliosababisha vifo vingi katika historia ya jimbo la magharibi la Marekani. Moto ambao umeua watu 56 karibu na mji wa Paradise, katika Kaunti ya Butte, kaskazini mwa mji mkuu wa Sacramento.

Ikulu ya White House ilitangaza siku ya Alhamisi kuwa Donald Trump atazuru jimbo hilo Jumamosi Novemba 17 na kukutana na watu walioathiriwa na moto. Rais Donald turm alitangaza hali ya "janga kubwa" kwa maeneo yaliyoathirika kwa moto, baada ya kuzua utata akishtumu Jimbo la California, linalotawaliwa na Democrats kushindwa kusimamia urasibu wa misitu wakati hifadhi ya misitu nchini Marekani iko chini ya mamlaka ya serikali kuu ya Washington.

Polisi wa Kaunti ya Butte imetoa orodha ya watu 300 ambao bado hawajapatikana. Kwa mujibu wa Mkuu wa Kaunti hiyo, Kory Honea, baadhi wanaweza kuwa wamepewa hifadhi na familia zao au marafiki lakini wengine inawezekana kuwa walifariki dunia.