MAREKANI-MEXICO-USALAMA-WAHAMIAJI

Mexico: Msafara wa wahamiaji wawasili kwenye mpaka wa Marekani

Wahamiaji wakifanya maombi yao Tijuana Novemba 15, 2018.
Wahamiaji wakifanya maombi yao Tijuana Novemba 15, 2018. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Baada ya mwezi mmoja wakiwa njiani kuelekea Marekani, hatimaye msafara wa wahamiaji kutoka Amerika ya Kati umewasili tangu siku ya Alhamisi huko Tijuana, nchini Mexico, kwenye mpaka na Marekani, licha ya vitisho vya Rais Donald Trump na kupelekwa kwa maelfu ya askari wa Marekani kwenye mpaka wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mapema asubuhi, mabasi ishirini na mbili yakiwa yamebeba wahamiaji 800 waliwasili karibu na mji huo unaopaikana katika Jimbo la Mexico la Baja California. Idadi hii imejiongeza idadi nyingine ya watu wengine 800 ambao tayari wamewasili katika makundi madogo tangu Jumapili.

"Najisikia vizuri, licha ya kuwa nimechoka. Ni mwezi mmoja sasa tangu nianze safari yangu nikiambatana na wasichana wangu wenye umri wa miaka 7, 11, 13 na 15," Miriam, 32, kutoka Honduras, 32, ameliambia shirika la Habari la AFP.

Wahamiaji wengine zaidi ya 3,000 wako njiani wakisafiri kwa basi wakielekea mji huo, ambako wanatarajia kuwasili jioni.

Wahamiaji wengi ni kutoka Honduras, ambao wanakimbia umasikini na machafuko yanayoendelea katika nchi yao.

Waliondoka Oktoba 13 katika mji wa San Pedro Sula.