MAREKANI-TRUMP-HAKI

Jaji wa Mahakama ya Juu Marekani akosoa kauli ya Donald Trump

Jaji Elena Kagan anaongea na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Marekani John Roberts nje ya Mahakama Kuu baada ya sherehe ya uzinduzi Washington, DC, Oktoba 1, 2010.
Jaji Elena Kagan anaongea na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Marekani John Roberts nje ya Mahakama Kuu baada ya sherehe ya uzinduzi Washington, DC, Oktoba 1, 2010. Photo: Larry Downing / Reuters

Jaji wa Mahakama ya Juu nchini Marekani John Roberts amemshutumu rais Donald Trump kwa kutoa matamshi yanayoingilia uhuru wa Mahakama hiyo, baada ya kumwita jaji mmoja wa mahakama hiyo kuwa ni mfuasi wa Barack Obama.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Jaji Roberts inakuja, baada ya Jaji mmoja, kuamua kuwa ilikuwa ni sahihi kwa wahamiaji kupewa hifadhi nchini Marekani, licha ya pingamizi kutoka kwa rais Trump.

Uamuzi huu ulimkasirisha Trump ambaye amesema Jaji huyo ni wa Obama, akiwa anamaanisha kuwa aliteuliwa na rais aliyemtangulia.

Kiongozi wa Mahakama hiyo, amesema hakuna Jaji wa Obama, Trump , Bush wala Clinton bali, Majaji waliopo ni wale wanaofanya kazi kwa umahiri kwa kuzingatia haki na sheria.

Licha ya shutuma hizi, rais Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa Jaji Roberts alikosea.

Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu kuingia kwenye majibizano ya maneno kuhusu uamuzi uliofanywa na mmoja wa Majaji nchini humo.