Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA-ULINZI

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis ajiuzulu

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis amechukua uamuzi wa kujiondoa kwenye wadhifa wake..
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis amechukua uamuzi wa kujiondoa kwenye wadhifa wake.. REUTERS/Francois Lenoir
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Matis ameamua kujiuzulu. Jim Mattis anajiuzulu kwenye wadhifa huo siku moja baada ya Donald Trump kutangaza kuondoa askari wa Marekani nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Mattis amekuwa akipinga kuondolewa kwa askari hao. Kama kawaida yake, Rais Donald Trump ametangaza kujiuzulu kwa waziri wake wa ulinzi kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hata hivyo Donald Trump amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na Jenerali Mattis.

Jenerai Mattis amekuwa akitetea uhusiano mzuri na washirika wa Marekani, huku akisema ana wasiwasi kwa yale yatakayowakuta Wakurdi baada ya kuondoka askari wa Marekani nchini Syria.

Kuondoka kwa askari wa Marekani nchini Syria, kwa upande wake ni jambo lisilowezekana.

Baadhi ya maseneta kutoka chama cha Republican ikiwa ni pamoja na Lindsey Graham wameonekana kumuunga mkono Jenerali Mattis kwa uamuzi wake huo na kusema hawaungi mkono askari wa Marekani kuondoka nchini Syria.

Imedhihirika kuwa Donald Trump hakuwa anamsikiliza tena waziri wake wa ulinzi. Siku ya Alhamisi Desemba 20 Jim Mattis alienda ikulu ya White House kujaribu kumshawishi rais Donald Trump kuacha kuondoa askari wa Marekani nchini Syria, bila mafanikio.

Vyombo vya habari kadhaa vya Marekani vimetangaza kwamba Rais Donald Trump anajiandaa kuondoa askari wa Marekani nchini Afghanistan. Awali alijaribu kufanya hivyo, lakini Jenerali Mattis alimshawishi kuachana na mpango huo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.