MAREKANI-MEXIOCO-USHIRIKIANO

Trump aomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na Mexico

Rais Donald Trump wakati wa hotuba yake kwa taifa, Jumatatu, katika ikulu ya White House.
Rais Donald Trump wakati wa hotuba yake kwa taifa, Jumatatu, katika ikulu ya White House. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani, Donald Trump ametaka kupewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta mrefu kwenye mpaka wa nchi hiyo na Mexico, akisema ukuta huo utasaidia kupunguza hali tete ya kibinadamu na kuimarisha usalama.

Matangazo ya kibiashara

Akihutubia taifa kupitia televisheni rais Trump amewakashifu wabunge wa Democrats kwa kuendelea kukwamisha mpango wake, akiwaita wasaliti waliotayari kuona wananchi wa taifa hilo wakiendelea kutaabika.

Saa chache baada ya hotuba yake, viongozi wa Democrats wamejitokeza na kumkosoa vikali rais Trump wakimtaka afungue shughuli za Serikali mapema iwezekanavyo.

Rais Donald Trump ameapa kuendelea na mipango yake ya kujenga ukuta wa urefu wa kilomita 3000 kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico.

Ukuta huo utakuwa na urefu wa kati ya mita 9 na 16 na utajengwa kwa kutumia changarawe.

Warepublican na wafuasi wao wanasema kuwa ukuta huo utawazui raia wa Mexico wanaoingia Marekani kinyume na sheria.

Mpaka kati ya Marekana na Mexico una umbali wa kilomita 3000.