VENEZUELA-SIASA

Spika wa bunge azuiliwa Venezuela

Juan Guaido, Spika wa Bunge la Venezuela.
Juan Guaido, Spika wa Bunge la Venezuela. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Mwanasiasa wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido, ambaye pia ni Spika wa Bunge amekamatwa kwa muda wa saa kadhaa na baadae kuachiliwa huru na maafisa wa idara ya upelelezi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili Juan Guaido alitoa maeneo makali ya wale anaowaita kuwa ni maadui wa taifa.

Siku ya Ijumaa, Juan Guaido alikuwa ametangaza hadharani kwamba yuko tayari kuchukua nafasi ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro, ambaye anaonekana zaidi kutengwa.

Maneno yake yalipelekea baadhi ya wafuasi wa upinzani kuhakikisha kuwa amejitangaza kuwa rais wa mpito, na pia aliwataja maafisa kadhaa wa serikali akitaka wafunguliwe mashitaka kwa kosa la uhaini.

Siku ya Jumapili, maafisa wa upelelezi walimkamata na kumuondoa katika gari lake alipokuwa akitoka mji mkuu Caracas akielekea mji wa pwani wa Caraballeda, mke wake na wabunge wa upinzani wamesema. Aliachiliwa huru saa chache baadae, wameendelea.

"Nataka kutoa ujumbe kwa Miraflores: hali imebadilika," Bw Guaido alisema katika mkutano wa kisiasa, mbele ya wafuasi wake. "Hapa sisi, hatuogope!"

Waziri wa Habari Jorge Rodriguez amesema kwenye runinga ya taifa kuwa kukamatwa kwa Juan Guaido hapa kuwa na "utaratibu" kitendo ambacho kilifanywa na maafisa wasio kuwa na nidhamu ambao walitaka kusaidia upinzani "kufikisha malalamiko yao mbele ya vyombo vya habari". Ameongeza kuwa maafisa ambao walishiriki katika kukamatwa kwa Guaido wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Rais Nicolas Maduro aliapishwa siku ya Alhamisi kwa muhula wa pili kuongoza Venezuela, nchi ambayo inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa na kiuchumi, ambapo katika miezi ya hivi karibuni imekumbwa na mgogoro wa kibinadamu, huku raia wengi wa nchi hiyo wakiendelea kukimbilia katika nchi jirani.