VENEZUELA-SIASA

Juan Guaido ajitangaza rais wa Venezuela, Maduro avunja uhusiano na Marekani

Juan Guaido s'est autoproclamé «président par intérim» du Venezuela mercredi 23 janvier à Caracas.
Juan Guaido s'est autoproclamé «président par intérim» du Venezuela mercredi 23 janvier à Caracas. © REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Sintofahamu inaendelea nchini Venezuela saa chache baada ya Spika wa Bunge Juan Guaido kujitangaza rais wa mpito wa nchi hiyo, huku rais Maduro akisema yeye ndio rais halali wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo jeshi la Venezuela limekataa kumtabua Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela, kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi Vladimir Padrino: "Hatua aliyochukuwa Juan Guaido inalenga kuzorotesha usalama na amani Venezuela. Sisi, askari wazalendo, hatukubali rais anayejificha kwenye kivuli kwa kutetea maslahi yasioyoeleweka au mtu kujitangaza rais kinyume na sheria. Jeshi linalinda Katiba yetu na ni katiba hiyo ndio sheria mama na msingi wa uhuru wa taifa hili. "

Wakati huo huo Nicolas Maduro ambaye anasema bado ni rais wa venezuela anayetambuliwa na katiba, ametangaza kuwa nchi yake imevunja uhusiano na Marekani, akiishtumu nchi hiyo kwamba inalenga kupindua kimabavu utawala wake.

Upinzani nchini Venezuela ambao uliwatolea wito raia wa nchi hiyo kumiminika mitaani kwa wingi Jumatao wiki hii kupinga serikali ya Nicolas Maduro, unasema kuwa muhula wa pili wa rais Maduro si halali.

Katika taarifa yake, Bunge la Venezuela linabaini kwamba Maduro, aliye chaguliwa tena katika uchaguzi uliosusiwa na vyama vikuu vya upinzani, ni "mwizi" wa madaraka.

Juan Guaido, anatarajia kuwaunganisha wapinzani wa mrithi wa Hugo Chavez (Nicolas Maduro) na amesema yuko tayari kukaimu nafasi yake, kwa msaada wa jeshi, muda wa kuandaa uchaguzi huru.

Juan Guaido, 35, ambaye anaungwa mkono na Marekani, anajiona kama mrithi wa Leopoldo Lopez, mtu wake wa karibu, kiongozi wa mwisho aliyeunganisha upinzani, ambaye alikamatwa mnamo mwaka 2014.

Katika ujumbe wake kwa raia wa Venezuela, Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence, siku ya Jumanne, alimtaja Maduro kama "dikteta asiye kuwa na uhalali wa kutawala."

Nchi kadhaa za Amerika kusini zimesem akuwa zinamtambuwa Juan Guaido kama rais awa mpito wa venezuela.

Hata hivyo Cuba na Mexico vimebaini kwamba vinamtambua Nicolas Maduro kama rais wa nchi ambayo inaendelea kukumbwa na sintofahamu.

Maandamano ya kupinga utawala wa Rais Nicolas Maduro, Januari 23, 2019.
Maandamano ya kupinga utawala wa Rais Nicolas Maduro, Januari 23, 2019. © REUTERS/Carlos Garcia Rawlins