VENEZUELA- MAANDAMANO-SIASA

Ufaransa yaomba wanahabari wawili kuachiliwa huru Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro apoteza imani kwa bunge la Ulaya.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro apoteza imani kwa bunge la Ulaya. REUTERS/Manaure Quintero

Waandishi wa habari watatu kutoka shirika la Habari la Uhispania la EFE na dereva wao, raia wa Venezuela, wamekamatwa nchini humo tangu Jumatano wiki hii, EFE imetangaza siku moja baada ya wanahabari wengine wawili kutoka Ufaransa wanaotoa makala ya kila siku kwenye kituo cha TMC kukamatwa.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Ufaransa, Wizara ya Mambo ya Nje imeomba waandishi hao wawili wa habari, ambao walikuwa wakiendesha kazi yao ya uandishi kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Waandishi wa habari watatu wa shirika la Habari la EFE ni mpiga picha, raia wa Colombia, Leonardo Muñoz, alikamatwa wakati akiripoti kuhusu maandamano dhidi ya serikali na mwandishi wa habari kutoka Uhispania, Gonzalo Dominguez Loeda, pamoja na mtayarishaji wa makala kwenye runinga ya Colombia, Mauren Barriga Vargas, ambao walikamatwa katika hoteli walikokuwa wakiishi.

Mkuu wa ofisi ya EFE katika nchini Venezuela, Nelida Fernandez, amesema wote watatu waliwasili mjini Bogota, nchini Colombia, mwezi huu wa Januari.

Serikali ya Uhispania na Mkuu wa sera za kidilpomasia wa Ulaya, Federica Mogherini, wameomba waandishi hao wa habari kuachiliwa huru mara moja.

"Tunaamini kwamba waandishi wa habari wanapaswa kutekeleza haki zao, kuendesha kazi yao," Mogherini amesema kando ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa ulaya huko Bucarest.