VEBEZUELA-SIASA

Maduro afutilia mbali muda wa mwisho uliyowekwa na nchi za Ulaya

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akisubiri zoezi la kijeshi huko Turiamo Februari 3, 2019.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akisubiri zoezi la kijeshi huko Turiamo Februari 3, 2019. Miraflores Palace/Handout via REUTERS

Rais wa Venezuela aliye chaguliwa Nicolas Maduro amefutilia mbali muda wa mwisho uliyowekwa na nchi kadhaa za Ulaya ambazo zinaomba kufanyika haraka uchaguzi mpya wa urais, la sivyo zitamtambua Juan Guaido kama rais wa Venezuela.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo rais Nicolas Maduro amesema yuko tayari kushirikia na anaunga mkono mkutano wa Montevideo.

Rais Maduro ameendelea kupata shinikizo kutoka nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majirani zake wa Amerika ya Kusini.

Katika mahojiano na kituo cha runinga cha Uhispania cha La Sexta, Nicolas Maduro amesema hawezi "kusalimu amri kutokana na shinikizo" kutoka kwa wale wanaotaka ajiuzulu na kumuunga mkono mpinzani wake Juan Guaido.

"Uchaguzi wa urais utafanyika tarehe iliyopangwa mnamo mwaka 2024, amesema Nicolas Maduro. Haijalishi kauli ya Ulaya kuhusu Venezuela. Ulaya inapawa kushughulikia matatizo yake: ukosefu wa ajira, ukuaji, wahamiaji. Ulaya haina hoja ya kuingilia kati katika masuala ya ndani ya Venezuela."

Siku ya Jumapili Uhispania, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Uholanzi, Ureno, pamoja na Austria, wawameutaka utawala wa Nicolas Maduro kuitisha haraka uchaguzi wa urais, la sivyo watamtambuwa Spika wa bunge Juan Guaido kama rais wa Venezuela.

Hivi karibuni Juan Guaido alijitangaza rais wa mpito wa Venezuela.