MAREKANI-SIASA-UCHUMI

Donald Trump aahidi kuwa ukuta utajengwa na atoa wito kwa maelewano

Donald Trump wakati wa hotuba yake kuhusu Muungano, Jumanne, Februari 5, 2019.
Donald Trump wakati wa hotuba yake kuhusu Muungano, Jumanne, Februari 5, 2019. Doug Mills/Pool via REUTERS

Katika hotuba yake kuhusu hali ya muungano mbele ya bunge la Congress Jumatano jioni, rais wa Maekani Donald Trump, kwa muda mrefu amerejelea mpango wake wa ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na Mexico, akibaini kwamba ndio njia pekee kwa usalama wa nchi yake.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani ametoa wito kwa wananchi wake kuwa na umoja.

Rais wa Marekani ameahidi tena, katika hotuba yake kuhusu hali ya mmungano mbele ya bunge la Wawakilishi na bunge la Congress kwamba atajenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico ili kupambana dhidi ya wahamiaji haramu.

Mradi huu huenda ukamdhoofisha kisiasa, kwa kuwa tayari amepoteza uungwaji mkono kutoka wabunge walio wengi wa chama cha Democratic. Baada ya siku 35 ya kukwama kwa shughuli za serikali nchini Marekani, Donald Trump alilazimika kufungua taasisi za shirikisho, bila hata hivyo kupata dola hata moja ya kujenga ukuta wake.

Wakati huo huo, ametoa wito kwa bunge la Congress kuwa na"maelewano" kati ya pane mbili ili kupata dola bilioni 5.7 anazohitaji.

"Utawala wangu umefanya pendekezo nzuri kwa Congress kukomesha mgogoro kwenye mpaka wetu wa kusini. Pendekezo hili linajumuisha msaada wa kibinadamu, kutokuwa na vikosi vya usalama kwenye mpaka, vifaa vya kugundua madawa ya kulevya, na kadhalika, " amesem araisa wa Marekani.

Mkutano na Kim Jong-un Februari 27 na 28

Rais Trump pia alitumia fursa kwenye mkutano huu wa kila mwaka kutangaza tarehe na mahali pa mkutano wake ujao na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Donald trump amesema mkutano kati yake na Ki Jong-un utakuwa Februari 27 na 28 nchini Vietnam.

Donald Trump pia ameonya kwa mara nyingine China kuwa haiwezi "kuiba ajira na utajiri wa Wamarekani," akitoa wito kwa Beijing kufanya "mabadiliko ya kimiundo" ili kukomesha biashara "isiyofuata sheria".