Mkutano wa kimataifa kuhusu mgogoro wa Venezuela kufanyika Montevideo

Maandamano ya kumuunga mkono Juan Guaido, Caracas, Februari 2, 2019.
Maandamano ya kumuunga mkono Juan Guaido, Caracas, Februari 2, 2019. REUTERS/Luisa Gonzalez

Mkutano wa kimataifa katika kujaribu kuondokana kwa amani na mgogoro wa venezuela unatarajia kufanyika katika mji mkuu wa Uruguay, Montevideo.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya, nchi nanae zilizotangaza kuwa zinamtambuwa Juan Guaido kama rais wa mpito wa Venezuela na nchi tano kutoka ukanda wa Amerika Kusini: Uruguay, Mexico, Costa Rica, Equador na Bolivia zinashiriki mkutano huo. Jitihada hizi zilizinduliwa na nchi mbili ambazo zinadai kuwa haziegemei upande hata mmoja, Uruguay na Mexico, wiki mbili zilizopita

Lengo la mkutano huo ni kujaribu kuweka mazingira yanayohitajika kwa kuepo kwa mazungumzo yenye lengo la kuondokana kwa amani na mgogor huo wa kisiasa na kijamii, mgogoro ambao una madhara makubwa kwa bara la Amerika.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje ya Uruguay, lengo ni kuweka kwa wadu wote wa mgogoro wa Venezuela njia ambayo itawezesha mazugumzo ya haraka ambayo yanaweza kukomesha mgogoro huo kwa njia ya amani na ya kidemokrasia. Hakuna mwakilishi kutoka upand wa utawaa wa Nicolas Maduro au upande wa Juan Guaido aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela.