MEXICO-USAAMA

Mexico: Miili 69 yafukuliwa katika makaburi ya halaiki Tecoman

Takriban umbali wa maili 650 kati ya maili 1,100 (1,770km) za mpaka wa Mexico na Marekani tayari kumejengwa ua au ukuta.
Takriban umbali wa maili 650 kati ya maili 1,100 (1,770km) za mpaka wa Mexico na Marekani tayari kumejengwa ua au ukuta. REUTERS/Hannah McKay

Makaburi mengi ya haliaki yamegunduliwa katika mji wa Tecoman, katika jimbo la Colima, ambapo miili 69 imefukuliwa. Mamlaka inachunguza miili hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Jimbo la Colima, kwenye pwani ya Pasifiki, ni jirani na Jalisco na Michoacan, kunakosafirishwa biashara ya madawa ya kulevya hadi Marekani.

Takriban umbali wa maili 650 kati ya maili 1,100 (1,770km) za mpaka wa Mexico na Marekani tayari kumejengwa ua au ukuta.

Trump aliahidi kujenga ukuta mrefu lakini walanguzi wamekuwa wakitumia ubunifu katika kutumia njia za kufikisha madawa Marekani.

Miongoni mwa njia hizi ni kutumia ndege ndogo zisizo na marubani na wakati mwingine kuchimba njia za chini kwa chini zinazofika hadi Marekani.

Mwezi Machi 2017, maafisa waligundua njia ya chini kwa chini ya umbali wa mita 380 ambayo ilikuwa imetoka kwenye mgahawa mmoja Mexico hadi kwenye jumba moja California.

Wiki iliyopita, Rais wa Mexico Andrès Manuel Lopez Obrador alizindua kampeni ya kitaifa ya kuwapata watu 40,000 waliotoweka.