HAITI-HAKI

Wafungwa 78 watoroka jela kusini mwa Haiti

Maafisa wa polisi wakipiga doria katika mitaa ya Port-au-Prince, mji unaokumbwa na maandamano kwa karibu wiki moja (picha ya kumbukumbu).
Maafisa wa polisi wakipiga doria katika mitaa ya Port-au-Prince, mji unaokumbwa na maandamano kwa karibu wiki moja (picha ya kumbukumbu). HECTOR RETAMAL / AFP

Wafungwa 78 wa jela la mji wa Aquin, kusini mwa Haiti, wametoroka jela tangu Jumatanne mchana, Februari 12, msemaji wa polisi amesema. Kwa mujibu wa polisi ya Haiti, uchunguzi umeanzishwa ili kujua sababu ya kutoroka kwa wafungwa 78 wa jela ya Aquin.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi, maandamano dhidi ya rais wa Haiti Jovenel Moïse yalifanyika mbele ya kituo cha polisi karibu na jela. Karibu wiki moja sasa, maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana, wakati mwingine maandamano yalikuwa yakigubikwa na vurugu, katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince na katika mikoa mingine wakiombarais Jovenel Moise ajiuzulu .

Mashirika ya haki za binadamu yamekuwa yakikosoa mazingira wanakozuiliwa wafungwa katika jela mbalimbali nchini Haiti.

Mashirika hayo yanashtumu wingi kupita kiasa wa wafungwa katika magereza, ukosefu wa usafi, ukosefu wa lishe na huduma. Kutowajibika kwa majaji ni mnoja ya sababu ya hali hiyo, mmoja wa wanaharakati wa haki za binadamu amesema.

Mnamo Oktoba 2018, ripoti ya uchunguzi wa shirika moja la haki za binadamu nchini Haiti ilibaini kwamba robo tatu ya watu 11,839 wanaozuiliwa nchini Haiti walikuwa bado wakisubiri uamuzi wa mahakama, baadhi wakizuiliwa kwa zaidi ya miaka kumi.