MAREKANi-SANDERS-SIASA

Bernie Sanders kuwania kiti cha urais Marekani

Seneta Bernie Sanders (kwenye picha.
Seneta Bernie Sanders (kwenye picha. REUTERS/Yuri Gripas

Seneta Bernie Sanders, 77, anajiandaa kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020 nchini Marekani. Jumanne wiki hii Bw Senders amesema kuwa atawania katika uchaguzi wa ndani wa chama cha Democratic ili kutafuta tiketi ya kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.

Matangazo ya kibiashara

Bernie Sanders alishindwa wakati wa kinyang'anyiro cha urais katika uchagui wa ndani wa chama cha Democratic, baada ay Hillary Clinton kuibuka mshindi na kupeperusha bendera ya chama hicho.

Katika uchaguzi wa ndani ya chama alishinda katika Majimbo 23.

Ametangaza kuwa atawania kiti cha urais kwenye barua pepe kwa wafuasi wake mapema Jumanne wiki hii.

"Kampeni yetu inalenga kuweka serikali na uchumi mikononi idadi kubwa ya watu, sio wachache," ameandika Bw Sanders.

"Kwa pamoja, nyinyi na mimi, tulianza katika kampeni ya mwaka 2016 mapinduzi ya kisiasa. Kwa sasa wakati umewadia kukamilisha mapinduzi hayo na kujadili kilichosababisha tunashindwa."

Ameelezea kuanzishwa kwa mfumo wa bima ya afya na kuongeza mshahara wa chini. "Miaka mitatu imepita (...) na sera hii sasa imeungwa mkono na Wamarekani wengi," Bernie Sanders ameongeza.