VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Venezuela yafunga mpaka wake na Brazil

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akizungumza wakati wa mkutano na wajumbe wa serikali  Caracas, Venezuela, Februari 13, 2019.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akizungumza wakati wa mkutano na wajumbe wa serikali Caracas, Venezuela, Februari 13, 2019. Miraflores Palace/Handout via REUTERS

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameamuru kufungwa kwa mpaka wa kusini mwa nchi yake, ambao unaitenganisha na Brazil. Hatua hii imeanza kutumika usiku wa kuamkia leo (saa za Venezuela).

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umechukuliwa kutokana na kile rais wa Venezuela amekiita "uchokozi" kutoka serikali ya mrengo wakulia ya Brazil.

Venezuela pia inafuatilia kwa karibu hali kwenye mpaka wake na Colombia, rais wa Venezuela ameongeza.

"Sitaki kuchukuwa aina hiyo ya maamuzi, lakini ninajifunza uwezekano wa kuchukuwa hatua kama hiyo, kufunga mpaka wa Venezuela na Colombia," amesema Maduro.

Colombia na Brazil wamejiunga na upinzani wa mrengo wa kulia nchini Venezuela kwa msimamo wao mmoja wa kumtimuwa rais Maduro na chama ccha Kisoshalisti cha PSUV.