VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Maduro ashtumu Marekani kutaka kuanzisha vurugu Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akiwahutubia wafuasi wake jijini Caracas, Februari 23, 2019.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro akiwahutubia wafuasi wake jijini Caracas, Februari 23, 2019. Yuri CORTEZ / AFP

Rais wa Venezuela Nocolas Maduro ameituhumu serikali ya Marekani kwa kupanga njama za kutengeneza mzozo nchini mwake ili kuanzisha vita katika taifa hilo la Amerika ya Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya Maduro ameyatoa saa chache tu baada ya makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence kutangaza vikwazo vipya dhidi ya washirika wa serikali ya rais Maduro wakati alipokutana na viongozi wa mataifa ya Amerika kusini akiwemo kiongozi wa upinzani Juan Guaido nchini Colombia.

Mike Pence alimwambia Juan Guaido kwamba Marekani inamuunga mkono katika harakati zake na itaendelea kumsaidia.

Wakati huo huo Mataifa ya Kusini mwa Amerika wametupilia mbali hoja ya kuishambulia kijeshi Venezuela, yakibani kwamba mzozo wa Venezuyela utatatuliwa kwa njia ya amani na kidiplomasia.

Hata hivyo nchi hizo zimesem akuwa zinamuunga mkono Juan Guaido na kumtambua kama rais wa mpito wa Venezuela.