MAREKANI-COHEN-HAKI-SIASA

Mwanasheria wa zamani Michael Cohen amgeukia Trump

Mwanasheria wa zamani wa Trump Michael Cohen akula kiapo kabla ya kusikilizwa mbeke ya bunge la wawakilishi, Februari 27, 2019.
Mwanasheria wa zamani wa Trump Michael Cohen akula kiapo kabla ya kusikilizwa mbeke ya bunge la wawakilishi, Februari 27, 2019. REUTERS/Jonathan Ernst

Michael Cohen, mwanasheria wa zamani wa rais wa Marekani Donald Trump amemgeukia mteja wake wa zamani akidai aliratibu mipango ya siri kwa ujenzi wa jengo kubwa, hata wakati alikana kuhusika na biashara yoyote Urusi, huku akimuita "mbaguzi", "tapeli" na "muongo".

Matangazo ya kibiashara

Michael Cohen, ametoa ushuhuda huo mbele ya Bunge la Wawakili Jumatano hii, Februari 27.

Cohen ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani, hasa kwa kudanganya mbele ya bunge, alitoa nyaraka kadhaa ikiwa ni pamoja na nakala ya hundi mbili zilizosainiwa na Donald Trump baada ya kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Marekani kwa kuwalipa wanawake wawili fedha kama kuwanyamanzisha juu ya uhusiano wao wa kimapenzi.

Katika taarifa yake ya ufunguzi,Michael Cohen alimkariri Donald Trump ambaye alimtumikia kwa zaidi ya muongo mmoja na kuelezea masikitiko yake kuona liweza kumtumikia. "Ninasikitikia siku niliyosema ndiyo kwa Bw Trump," Cohen amesema.

"Ninasikitikia msaada niliotoa na ambao unaendelea kumpa kibri. Nijutia makosa yangu, na nimekubali hadharani kutowajibika kwangu na nakiri kuwa nimekosea katika Wilaya ya Kusini mwa New York.

Ameeleza pia kwamba Trump alifahamu kuhusu kufichuliwa kwa barua pepe zilizodukuliwa za chama cha Democrat na amemuita kiongozi huyo "mbaguzi", "tapeli" na "muongo".

Donald Trump amesema kuwa Michael Cohen anadanganya ili kupunguza kifungo chake gerezani."

Hata hivyo Cohen alikikiri wazi kwamba Donald Trump hana biashara yoyote na Urusi.