BRAZILI-TEMER-HAKI

Rais wa zamani wa Brazili Michel Temer aachiliwa huru

Rais wa zamani wa Brazili Michel Temer anakabiliwa na madai ya rushwa.
Rais wa zamani wa Brazili Michel Temer anakabiliwa na madai ya rushwa. REUTERS/Ueslei Marcelino

Rais wa zamani wa Brazili Michel Temer yuko huru tangu Jumatatu usiku. Aliachiliwa huru kutoka kituo cha Polisi cha Rio de Janeiro ambako alikuwa kizuizini tangu kukamatwa kwake Alhamisi wiki iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Alikamatwa kwa madai ya kashfa ya rushwa, baada ya mahakama ya rufaa ya shirikisho kuchukuwa uamuzi wa kumuachilia huru mapema mchana.

Jaji Ivan Athié amebaini kwamba ushahidi uliotolewa na wachunguzi haujaeleza umuhimu wa "kuwekwa kizuizini" Michel Temer na watuhumiwa wengine saba, ikiwa ni pamoja na Waziri wa zamani Wellington Moreira Franco.

"Shutma zinazomkabili ni za zamani, ikiwa ni pamoja na vitendo visivyo halali ambavyo vilifantwa kinyume cha sheria, lakini hakuna ushahidi wa uhalifu tangu mwaka 2016 au mambo mengine yanayothibitisha kuzuiliwa jela," Jaji Ivan Athie ameandika katika hukumu yake.

Katika taarifa yake, ofisi ya mwendesha mashitaka wa shirikisho imetangaza nia yake ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Michel Temer alikamatwa siku ya Alhamisi katika uchunguzi wa madai ya rushwa kuhusiana na ujenzi wa kituo cha umeme cha nyuklia Angra 3.

Waendesha mashitaka wanamshtumu Temer kusimamia "kundi la kihalifu" ambalo lilipitisha mlango wa nyuma reals bilioni 1.8 (sawa na euro milioni 415) kama rushwa kupitia mipango mbalimbali, hususan kuhusiana na ujenzi wa kituo cha umeme cha nyuklia Angra 3 jijini Rio de Janeiro na kwa makampuni ya umma.