Pata taarifa kuu
VENEZUELA-SIASA-UCHUMI

Kiongozi wa upinzani Venezuela aapa kuendelea na harakati za kumuondoa Maduro

Kiongozi wa upinzani  nchini Venezuela Juan Guaido.
Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido. REUTERS/Ivan Alvarado
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido amesisitiza kuwa hakuna kitachomzuia kuendeleza harakati za kumwondoa madarakani rais Nicolas Maduro.

Matangazo ya kibiashara

Ametoa kauli hii, muda mfupi baada ya wabunge wabunge wanaomuunga mkono rais Maduro, kumwondelea kinga ya kisiasa.

Mahakama Kuu ya Venezuela, ambayo iko chini ya udhibiti wa serikali ya rais wa Nicolas Maduro, iliomba kiongozi wa upinzani Juan Guaido, avuliwe kinga ya ubunge, ili aweze kufunguliwa mashitaka.

Jaji Mkuu aliagiza wabunge kufanya hivyo, baada ya Guaido kukiuka agizo la Mahakama la kutoondoka nchini humo.

Juan Guaido, ambaye ndiye Spika wa Bunge la Venezuela linalodhibitiwa na upinzani, anashutumiwa kukiuka marufuku aliyowekewa ya kuondoka nchini.

Mwanasiasa huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 35 alifutilia mbali uamuzi wa Mahakama Kuu wa Januari 29, akiondoka nchini kinyume cha sheria na kufanya ziara katika nchi jirani za Colombia, Brazili, Paraguay, Argentina na Ecuador, mwishoni mwa mwezi Februari hadi mwanzoni mwa mwezi Machi.

Uamuzi huu unakuja wakati Nicolas Maduro na mpinzani wake mkuu wanaendelea kupigania madaraka tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika nchi ambayo inakumbwa na kiza kinene kufuatia kukatwa kwa umeme.

Kiongozi huyo wa upinzani, anatambuliwa na Marekani na mataifa mengine ya Magharibi kama kiongozi wa nchi hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.