Pata taarifa kuu
BRAZILI-LULA-HAKI

Mahakama ya Brazil kutathmini rufaa ya Lula dhidi ya hukumu aliopewa

Rais wa zamani Lula (katikati) akisindikizwa na polisi alipofika kwenye makao makuu ya Polisi ya Shirikisho, Curitiba, (kusini mwa Brazil) baada ya kuhudhuria mazishi ya mjukuu wake Sao Paulo Machi 2, 2019.
Rais wa zamani Lula (katikati) akisindikizwa na polisi alipofika kwenye makao makuu ya Polisi ya Shirikisho, Curitiba, (kusini mwa Brazil) baada ya kuhudhuria mazishi ya mjukuu wake Sao Paulo Machi 2, 2019. © AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mahakama Kuu ya Haki nchini Brazil (STJ) inatarajia kutathmini rufaa ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva, dhidi ya hukumu ya kifungo cha miaka 12 jela kwa rushwa. Ni mwaka mmoja sasa tangu aanze kutumikia kifungo hicho.

Matangazo ya kibiashara

STJ inatarajia kutoa maamuzi yake kuhusu rufaa ya kufuta hukumu ya miaka 12 jela iliotolewa dhidi ya rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva, aliyetawala nchi hiyo kati ya miaka ya 2003 na 2010 katika mazingira ya kashfa kubwa ya rushwa kupitia kampuni ya mafuta ya serikali, Petrobras, mahakama imesema katika taarifa.

Lula, ambaye anazuiliwa jela tangu Aprili 7, 2018 katika gereza la Curitiba, kusini mwa Brazil, alihukumiwa na mahakama ya mwanzo na ya pili kuwa alipewa nyumba ya kifahari ya ghorofa katika mji wa Guaruja (pwani ya Sao Paulo Mashariki) nyumba ambayo ilitolewa kwa mikataba na kampuni ya Petrobras.

Mnamo mwezi Novemba, Jaji Felix Fischer wa Mahakama Kuu ya Haki, STJ, alikataa "rufaa maalum" ya Lula, lakini wanasheria wake waliomba jopo la majaji la mahakama hiyo kukutana kutathmini rufaa hiyo.

Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika leo Jumanne. Majaji wane kati ya watano watashiriki kikao hicho, na idadi hii ndio inayohitajika kwa kupitisha uamuzi.

Ikiwa idadi hii haitokamilika, kuna uwezekano wa kuitisha majaji kutoka Mahakama Kuu nyinge ya Haki kuja kusaidi kuchukuwa uamuzi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.