VENEZUELA-MAREKANi-MADURO-SIASA-USALAMA

Venezuela: Marekani yashinikiza Maduro kuachia madaraka

Wakati Juan Guaido aliitoa wito wa kuendelea na maandamano nchini Venezuela Jumatano hii, Mei 1, 2019, Marekani imeendelea kutoa shinikizo ili Nicolas Maduro aweze kuondoka madarakani, na hata kuondoka nchini.

Wafuasi wa upinzani wakikabiliana na vikosi vya usalama va Venezuela katika kambi ya kijeshi ya "La Carlota" Caracas.
Wafuasi wa upinzani wakikabiliana na vikosi vya usalama va Venezuela katika kambi ya kijeshi ya "La Carlota" Caracas. Reuters/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

"Sio jaribio la mapinduzi. Juan Guaido kujaribu kuchukua udhibiti wa jeshi haina uhusiano wowote na jaribio la mapinduzi, "amesema John Bolton, mshauri wa rais wa Marekani anayehusika na masuala ya usalama.

Wakati kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido ametoa wito kwa wafuasi wake kuendelea na maandamano, siku moja baada ya kujaribu kuingia mitaani na kuangusha utawala wa Maduro, jaribio ambalo lilishindwa, serikali ya Marekani inasema inafuatilia kwa uangalifu hali inayoendelea nchini Venezuela. Marekani inaendelea kushinikiza Nicolas Maduro kuondoka nchini.

Siku nzima ya Jumanne, viongozi wa Marekani waliendelea kuongeza shinikizo kwa utawala wa Maduro na nchi zinazomuunga mkono. Makamu wa rais Mike Pence na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, kwenye Twitter, walikuwa wakikaribisha operesheni ya "kujikomboa" iliyozinduliwa na Juan Guaido na kuthibitisha uungwaji wao mkono kwa mabadiliko ya amani kuelekea demokrasia.

John Bolton, kwa upande wake, amekumbusha kwamba mambo yote yanajadiliwa kuung'oa utawala wa Maduro, huku akimuonya Maduro kutumia nguvu dhidi ya raia.