MAREKANI-SIASA-HAKI

Spika wa bunge Marekani amnyooshea kidole cha lawama mwanasheria mkuu wa Serikali

Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi, amemtuhumu mwanasheria mkuu wa Serikali Bill Barr kwa kusema uongo bungeni, matamshi yanayozidisha sintofahamu zaidi katika sakata la kati ya utawala wa rais Donald Trump na wabunge wa Democrats.

Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi.
Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi. ©REUTERS/Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Pelosi ametoa kauli hii baada ya mwanasheria mkuu kutotokea kwenye mahojiano na kamati ya sheria ya Congress Alhamisi wiki hii.

Spika Pelosi amesema kilichofanywa na mwanasheria mkuu ni kosa la jinai na tayari ameonesha kuwa mtetezi namba moja wa rais Trump kuhusu ripoti ya Robert Mueller.

Wabunge wa Democrats wamepanga kutumia njia za kisheria kumshinikiza Barr atoe ripoti kamili ya Mueller ambayo haijachambuliwa na ofisi yake.