Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAN-JESHI-NYUKLIA

Marekani kutuma wanajeshi zaidi eneo la Mashariki ya Kati

Meli ya mafuta iliyoshambuliwa katika pwani ya ghuba ya Oman
Meli ya mafuta iliyoshambuliwa katika pwani ya ghuba ya Oman ©ISNA/Handout via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Marekani inasema itatuma wanajeshi wake 1,000 zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati, wakati huu hali ya wasiwasi ikiendelea kushuhudiwa kati yale na Iran lakini pia na mataifa mengine jirani.

Matangazo ya kibiashara

Kaimu Waziri wa Ulinzi Patrick Shanahan amesema hatua hii ni kwa sababu ya tabia aliyoeleza ni ya kukera inayooneshwa na wanajeshi wa Iran.

Hata hivyo, Marekani haijaweka wazi, ni wapi wanajeshi hao watapiga kambi.

Aidha, Jeshi la Marekani limetoa mkanda wa video unaonesha kuwa jeshi la Iran likishambulia meli za mafuta katika bahari ya ghuba ya Oman, madai ambayo Tehran imeendelea kukanusha.

Hatua hii imekuja baada ya Iran siku ya Jumatatu kutangaza kuwa haitatekeleza sehemu ya mkataba wa kusitisha mradi wake wa nyuklia uliotiwa mwaka 2015 kati yake na mataifa ya Magharibi, yakiongozwa na Marekani ambayo kwa sasa imejiondoa.

Tehran inasema kuanzia tarehe 27 mwezi Juni, itaanza kurutibisha tena uranium, hali ambayo inazua wasiwasi hasa kwa Marekani na Israel, mataifa ambayo yamekuwa yakishuku kuwa Iran inatengeza silaha za maangamizi ili kuzilenga.

China inaitaka Iran kuendelea kutekeleza mkataba huo wa nyuklia.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.