MAREKANI-SIASA-USALAMA

Donald Trump aagiza gwaride la kijeshi kufanyika Julai 4

Hatua hii ya Donald Trump inakuja baada ya kuhudhuria gwaride la jeshi la Ufaransa wakati wa maadhimisho ya uhuru Julai 14, 2017.
Hatua hii ya Donald Trump inakuja baada ya kuhudhuria gwaride la jeshi la Ufaransa wakati wa maadhimisho ya uhuru Julai 14, 2017. MANDEL NGAN / AFP

Rais wa Marekani amepanga kuwepo na gwaride la kijeshi, magari ya kivita ya kijeshi yakishirikishwa kwa kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Marekani, Alhamisi hii, Julai 4.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump anataka jeshi litumie vifaa vyake katika gwaride la siku ya kuadhimisha uhuru wa Marekani, siku ambayo inaadhimishwa Julai 4 kila mwaka.

Kwa mara ya kwanza magari ya makuu ya kivita yametakiwa kushiriki gwaride hilo.

Muda wa zoezi la kurusha itifaki utaongezwa baada ya ndege za kivita kualikwa kushiriki katika zoezi la Julai 4. "Nitasema maneno machache, siku hiyo tutashuhudia kwa macho yetu ndege za kivita zikipaa angani na kupita juu yetu," amesema rais wa Marekani.

Kwa upande wa chama cha Democratic chenye viti vingi bungeni, wanasema kwamba, hatua hiyo ya Donald Trump ni njia ya kuweka tukio hilo kwa manufaa yake, ikiwa imesalia karibu mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa urais wa 2020. Wabunge kutoka chama hicho wanataka pia kujua gharama ya tukio hili. Utawala wa Trump haujatoa jibu kwa swali hilo.

Viongozi wa Wilaya ya Columbia ambako kumepangwa kufanyika sherehe hizo wamesema mji wao haukukujengwa kwa kupokea vifaa kama hivyo, huku wakibaini kwamba magari makuu ya kivita ya kijeshi yataharibu barabara muhimu. "Magari hayo yatawekwa katika maeneo maalumu, amesema rais donald trump.

Hatua hii ya Donald Trump inakuja baada ya kuhudhuria gwaride la jeshi la Ufaransa wakati wa maadhimisho ya uhuru Julai 14, 2017.