MAREKANI-TRUMP-SIASA-USALAMA

Donald Trump azua sintofahmu kwa kuwashambulia baadhi ya wabunge wa Marekani

Mbunge kutoka chama cha Democratic Ocasio-Cortez, miongoni mwa wabunge wanne walioshambuliwa na rais Trump.
Mbunge kutoka chama cha Democratic Ocasio-Cortez, miongoni mwa wabunge wanne walioshambuliwa na rais Trump. REUTERS/Jeenah Moon

Rais wa Marekani Donald Trump amezua sintofahamu baada ya kundika ujumbe kwenye twitter akiwashambulia kwa maneno makali wabunge wanawake kutoka chama cha Democratic.

Matangazo ya kibiashara

"Inavutia kuona wabunge wa Democratic 'wanaotaka maendeleo' ambao waliwasili kutoka nchi ambazo serikali zake ni majanga matupu, zilizo mbaya zaidi, zilizo na kiwango kikubwa cha rushwa, na zisizojiweza kokote duniani (iwapo ni serikali zilizokuwa zinafanya kazi) sasa wakizungumza kwa ukali wakiwaambia watu wa Marekani, taifa kubwa na lenye nguvu duniani, namna tunavyostahili kuiendesha serikali yetu”, Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Kwanini wasirudi kusaidia kuyarekebisha mataifa yaliosambaratika na yaliogubikwa kwa uhalifu wanakotoka. Alafu warudi watuonyeshe namna inavyostahili kushughulikiwa”, ameongeza rais Trump.

Wabunge hao pamoja na bunge wengine kutoka chama cha Democraic na baadhi kutoka chama cha Republican wamelaani maneno hayo ya Trump wakiyataja maneo yake kama ya “kibaguzi.