VENEZUELA-MAZUNGUMZO-USALAMA-SIASA

Venezuela: Pande hasimu kuanza tena mazungumzo Barbados

Kiongozi wa upinzani wa Venezuela Juan Guaido na rais Nicolas Maduro.
Kiongozi wa upinzani wa Venezuela Juan Guaido na rais Nicolas Maduro. Yuri CORTEZ / AFP

Serikali ya Venezuela na upinzani wanatarajia kuanza tena mazungumzo Jumatatu hii, Julai 15 katika kisiwa cha Caribbean cha Barbados. Pande hizi mbili zilitamatisha duru ya kwanza ya mazungumzo Jumatano iliyopita zikubali kuanzishwa kwa jukwaa la mazungumzo ya kudumu.

Matangazo ya kibiashara

Hakujakua na taarifa kuhusu ajenda ya mazungumzo kati ya serikali na upinzani huko Barbados. Lakini kwa mujibu wa Norway, ambayo inasimamia mazungumzo hayo, ukimya huo ni muhimu ili kufikia mkataba wa kisiasa.

Hata hivyo, inafahamika kwamba mazungumzo yanahusu pointi sita, ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa uchaguzi wa urais na kurejeshwa kwa Bunge kama taasisi muhimu nchini. Bunge ambalo lilikuwa likidhibitiwa na upinzani lilifutwa na kurejelewa na jopo linaloundwa na wafuasi wa rais Nicolas Maduro.

Hatima ya rais Nicolas Maduro pia ni itajadiliwa katika mazungumzo hayo, kwa mujibu wa tovuti mbalimbali za habari.

Jina la gavana wa jimbo la Miranda, Hector Rodriguez, linapewa nafasi kubwa ya kurejelea Nicolas Maduro katika uchaguzi wa urais wa mapema unaotarajiwa kufanyika nchini humo hivi karibuni.

Mpinzani wake, Juan Guaido, aliyejitangaza rais wa mpito wa Venezuela, anasema yuko makini na hali hiyo. "Mikutano hii ni jitihada za Serikali ya Norway na siyo" mazungumzo" , Juan Guaido alisema mwishoni mwa wiki hii.

Bw Guaido amebaini kwamba "utaratibu" huu unalenga kupata uhakikisho wa Nicolas Maduro kuwa yuko tayari kuachia ngazi na kufanyika uchaguzi huru na wa wazi.