MAREKANI-SIASA-USALAMA

Trump ashtumiwa mbaguzi wa rangi na Baraza la Wawakilishi Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amekana shutuma dhidi yake kuwa yeye ni mbaguzi.
Rais wa Marekani Donald Trump amekana shutuma dhidi yake kuwa yeye ni mbaguzi. Brendan Smialowski / AFP

Baraza la Wawakilishi la Marekani limepitisha makubaliano ya pamoja yanayokemea kauli za "kibaguzi" za rais Donald Trump, shutma aliyotetea wakati akiendelea kuwashambulia vikali wabunge wanne wa chama cha Democratic kutoka jamii ya watu wachache nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Wawakilishi, lenye wabunge wengi kutoka chama cha Democratic, "linalaani vikali maneno ya kibaguzi yaliyoandikwa na rais Donald Trump yanayolalisha na kuzidisha hofu na chuki kwa wananchi wapya wa Marekani," imesema nakala hiyo.

Katika ukurasa wa Twitter, Rais Donald Trump aliwataka wanawake hao wasio na asili ya Marekani, ambao watatu walizaliwa nchini Maekani, ''kuondoka'' kuelekea kwenye nchi zao walipotoka.

Hata hivyo rais Trump amekataa shutuma kuwa yeye ni mbaguzi: ''sina asili ya ubaguzi mwilini mwangu!''.

Wakati huo huo amewatolea wito wabunge kutoka chama chake cha Republican kwamba wasianguki kwenye "mtego", uliotegwa na wapinzani wake."

Wakizungumza na waandishi wa habari wabunge hao wanawake wamesema, hivi sasa watu waweke akili zao kwenye sera za nchini Marekani na si maneno ya rais Trump.