MAREKANI-UTAFITI-UCHUMI

Miaka 50 baada ya mwanadamu kutembea mwezini

Buzz Aldrin akitembea mwezini karibu na chombo cha Eagle wakati wa ujumbe wa chombo cha anga Apollo 11 Julai 21, 1969.
Buzz Aldrin akitembea mwezini karibu na chombo cha Eagle wakati wa ujumbe wa chombo cha anga Apollo 11 Julai 21, 1969. Domaine public/Nasa/Neil A. Armstrong

Julai 21, 1969, watu milioni 600 walifuata moja kwa moja zoezi la chombo cha Appolo 11 kutua mwezini, na hatua ya kwanza ya binadamu, Neil Amstrong, kutua na kutembea mwezini.

Matangazo ya kibiashara

Miaka 50 iliyopita, mwanaanga wa Marekani, Neil Armstrong, alitua na kutembea mwezini, na hivyo kuwa mwanadamu wa kwanza kuchukua hatua hiyo.

Amstrong alisema wakati huo kuwa hatua aliyochukua yeye likuwa ndogo kwa mtu, lakini ilikuwa kubwa sana kwa binadamu wote.

"Hatua moja ndogo kwa mwanamume mmoja, hatua moja kubwa kwa binadamu."

Kwa kumpeleka mwanadamu mwezini, Marekani iliishinda Urusi katika mashindano ya kudhibiti anga za mbali.

Tarehe 21 Julai mwaka 1969 chombo cha anga, Apollo 11, kiliwapeleka angani wanaanga watatu wa Marekani, Neil Amstrong, Buzz Aldrin na Michael Collins. Licha ya matatizo ya kompyuta yaliyokuwepo, chombo cha Eagle kilifanikiwa kutua mwezini. Wanaanga walikabiliwa na chaguo, kugeuza na kurudia au kuendesha mitambo kwa mikono yao. Walitumia mikono yao kuendesha mitambo. Neil Armstrong alikuwa wa kwanza kuteremka na kutembea mwezini.

Watu zaidi ya nusu bilioni duniani kote walifuatilia tukio hilo kwenye televisheni miaka 40 iliyopita.

Mradi huo ulianza tarehe 25 mwezi Mei mnamo mwaka 1961 wakati rais John F. Kennedy aliposema " Marekani imechagua kwenda mwezini siyo kwa sababu ni rahisi kufanya hivyo, bali kwa sababu ni vigumu"

Huo ulikuwa wakati ambapo vita baridi baina ya Marekani na Urusi vilikuwa vikishamiri, na ambapo Urusi ilikuwa mbele katika utafiti wa anga.

Urusi ilikuwa ya kwanza kupeleka satelaiti angani na mwanaanga-Yuri Gagarin. Kutokana na hayo, Marekani ilipania kwa kila hali kumpeleka mwanadamu kwenye mwezi na ilifanikiwa.

Safari zingine tano zilifuatia. Kwa jumla, Wamarekani 12 wametua mwezini hadi sasa. Lakini shangwe zote zilitoweka haraka. Mmarekani wa mwisho kwenda mwezini alikuwa Eugene Cernon mnamo mwaka 1972. Baada ya hapo mradi wa Apollo ulimalizika.

Hata hivyo, wanaanga wa Marekani sasa wanatoa miito juu ya kutayarisha safari ya kwenda kwenye sayari ya Mars.