Trump amshambulia Mueller, kabla ya kuhojiwa na wabunge
Imechapishwa:
Rais wa Marekani amemshutumu Robert Mueller aliyeongoza uchunguzi wa iwapo Urusi iliingia Uchaguzi wa urais mwaka 2016, wakati huu anapotarajiwa kuhojiwa na wabunge wiki hii.
Wabunge wanatarajiwa kumhoji Mueller ambaye katika ripoti aliyoitoa baada ya uchunguzi wa miaka miwili, alibainisha kuwa Urusi iliingilia uchaguzi huo lakini haikuweza kuthibitisha iwapo Trump mwenyewe alihusika.
Rais Trump ameendelea kusisitiza kuwa ripoti hiyo ni ya uongo na kuongeza kuwa hatafuatilia mahoajino kati ya Mueller na wabunge hao.
Mwezi Machi mwaka huu ripoti ya Muller ilimsafisha Donald Trump.
Kampeni iliyoendeswa na rais wa Marekani Donald Trump 'haikushirikiana na Urusi wakati wa uchaguzi wa 2016, Kwa mujibu wa muhtasari wa ripoti hiyo iliyowasilishwa kwenye bunge la Congress mwezi Machi mwaka huu.
Wakati huo huo wakili wa Trump, Rudy Giuliani, alisema ripoti "ilikuwa bora kuliko nilivyotarajia ".