MAREKANI-URUSI-MUELLER-TRUMP-SIASA

Mueller: Ripoti yangu haijamsafisha Donald Trump

Aliyekuwa kiongozi wa timu ya wachunguzi kuhusu ikiwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016, Robert Mueller, amesisitiza kuwa ripoti yake haikumsafisha moja kwa moja rais Donald Trump.

Mwendesha Mashtaka Maalum wa zamani Robert Mueller akihojiwa na wabunge, Washington, Julai 24, 2019.
Mwendesha Mashtaka Maalum wa zamani Robert Mueller akihojiwa na wabunge, Washington, Julai 24, 2019. SAUL LOEB / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na wabunge wa kamati ya sheria na ile ya intelijensia ikiwa alimsafisha rais Trump dhidi ya tuhuma za kuingilia uchaguzi wake, Muller alilisitiza kuwa ripoti yake haikumsafisha.

Katika majibu yake ambayo alitegemea sana ripoti aliyowasilisha kwa wizara ya sheria nchini humo, Mueller amesema walishindwa kumfungulia mashtaka rais Trumop kutokana na utamaduni wa wizara ya sheria kutomshtaki rais aliyeko madarakani lakini haimaanishi hakukiuka sheria.

Wabunge wa Republican wanaomtetea rais Trump walimshambulia Mueller kwa upendeleo huku wale wa Democrats wakimuuliza maswali yaliyojaribu kuonesha kuwa rais Trump alikiuka sheria kwa kujaribu kuingilia uchunguzi wake.

Hata hivyo tipoti ya Mueller ilithibitisha Urusi kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016 kumsaidia rais Trump kushinda uchaguzi.