Adhabu ya kunyogwa kurudi kutekelezwa Marekani

Barr amesema wafungwa watano wanaotarajiwa kunyongwa walihukumiwa kwa makosa ya mauaji, ubakaji wa watoto na wazee.
Barr amesema wafungwa watano wanaotarajiwa kunyongwa walihukumiwa kwa makosa ya mauaji, ubakaji wa watoto na wazee. Brendan Smialowski / AFP

Serikali ya Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2003 inatarajia kutekeleza adhabu ya kunyonga baada ya kuwa imesitisha kwa muda wa karibu miaka 16, imesema taarifa ya mwanasheria mkuu wa Serikali.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake Mwanasheria Mkuu wa Serikali, William Barr, amesema ameiagiza idara ya magereza kupanga ratiba ya kunyongwa kwa wafungwa watano.

Barr amesema wafungwa hao walihukumiwa kwa makosa ya mauaji, ubakaji wa watoto na wazee.

Taarifa yake imesema baada ya majadiliano na mamlaka husika, wamekubaliana kuwa adhabu ya juu kwa wafungwa hao ni kunyongwa na kwamba Serikali itaendelea kuheshimu sheria za nchi kwa ajili ya kutenda haki kwa waathirika wa vitendo na wanafamilia.

Tayari mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yamekashifu uamuzi huo wa Serikali ya Marekani.