MAREKANI-URUSI-USALAMA

Marekani yajitoa kwenye mkataba wa nyuklia na Urusi

Marais Trump na Putin, Novemba 11, 2017, Danang, Vietnam, kwa mkutano wa APEC.
Marais Trump na Putin, Novemba 11, 2017, Danang, Vietnam, kwa mkutano wa APEC. REUTERS/Jorge Silva

Marekani imejitoa rasmi kwenye mkataba wa nyuklia iliyoafikiana na Urusi, ambao ulitiliwa saini mnamo mwaka 1987, na hivyo kutoa njia katika mbio mpya za ushindani wa silaha. Uamuzi huo umechukuliwa leo Ijumaa Agost 2, 2019.

Matangazo ya kibiashara

"Mkataba wa INF [FNI kwa Kifaransa] ulikuwa muhimu kwetu, lakini unafanya kazi tu ikiwa pande zote mbili zitauheshimu," Mkuu mpya wa majeshi ya Marekani, Mark Esper, alisema hivi karibuni. "Marekani itaheshimu mkataba huo na masharti yake yote hadi Agosti 2, baada ya hapo tutafanya kile kilio katika maslahi yetu," aliwaambia wajumbe wa bunge la Seneti.

Utaratibu wa kujiondoa, kwa upande wa Marekani, ulianzishwa mnamo mwezi Februari mwaka huu. Upande wa Urusi, Vladimir Putin alisahihisha mnamo Julai 3 kusimamishwa kwa ushiriki wa nchi yake kwenye mkataba huo na ukosefu wa mageuzi. Kujitoa kwa nchi hizo mbili kwenye mkataba huo kunasababisha mwisho wa mkataba wa INF.

Maafisa wakuu wa Jeshi la Urusi wakionyesha mfumo wa makombora ya 9M729, Moscow Januari 2019.
Maafisa wakuu wa Jeshi la Urusi wakionyesha mfumo wa makombora ya 9M729, Moscow Januari 2019. REUTERS/Maxim Shemetov

Mkataba huo unaohusu zana za nyuklia za masafa ya katikati (INF) ulisainiwa na rais wa Marekani Ronald Reagan na kiongozi wa iliyokuwa Sovieti Mikhail Gorbachev mnamo 1987.

Ulipiga marufuku makombora ya masafa ya kati ya kilomita 500-5,500.

Mwaka huu Marekani na Nato ziliishutumu Urusi kwa kukiuka makubaliano hayo kwa kufyetua aina mpya ya kombora, jambo ambalo Moscow inalikana.

Marekani imesema ina ushahidi kuwa Urusi imetuma kombora aina ya 9M729 linalofahamika kwa Nato kama SSC-8. Tuhuma hizi ziliwasilishwa kwa washirika wa Nato wa Marekani ambao wote waliunga mkono madai ya Marekani.