MAREKAN-TRUMP-RISASI-CHUKI

Watu 29 wapoteza maisha nchini Marekani katika matukio mawili ya kupigwa risasi

Duka la jumla lilishambuliwa katika jimbo la Texas
Duka la jumla lilishambuliwa katika jimbo la Texas Joel Angel JUAREZ / AFP

Watu 29 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 20  kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya kupigwa risasi yaliyotokea ndani ya saa 24 nchini Marekani, matukio ambayo yamezua wasiwasi kuhusu umiliki wa silaha nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi la kwnaza lilitokea katika duka la jumla la Walmart katika mji wa EL Paso, katika jimbo la Texas wakati, mtu aliyekuwa amejihami kwa bastola kuanza kuwafwatulia watu risasi na kuwauwa watu 20.

Baada ya saa 13, mtu mwingine aliyekuwa amejihami kwa bastola, aliwauwa watu wengine tisa katika mji wa Dayton katika jimbo la Ohio.

Haya ndio mauaji mabaya kuwahi kufanya kwa kipindi kifupi katika majimbo hayo mawili, na maafisa wa polisi wakisaidiwa na wake wa FBI, wanasema, wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini waliohusika.

Rais Donald Trump, amelaani mauaji haya na kusema vitendo hivyo ni vimetekelezwa na watu waoga na huenda ni chuki ndio iliyowaongoza kutekeleza mashambulizi hayo.

Miaka ya hivi karibuni, Marekan imeendelea kukabiliana na changamoto hii ya watu wanaomiliki bastola, kuzitumia visivyo na kuelekea Uchaguzi wa mwaka 2020, wanasiasa wameendelea kushinikiza kuwepo kwa sheria itakayosaidia kudhibiti umiliki wa silaha.