Pata taarifa kuu
MAREKANi-CHINA-BIASHARA

Donald Trump achukuwa hatua kuhusu ongezeko la kodi mpya kwa bidhaa kutoka China

Rais Donald Trump katika Ofisi yake ndogo, Washington, Septemba 11, 2019.
Rais Donald Trump katika Ofisi yake ndogo, Washington, Septemba 11, 2019. NICHOLAS KAMM / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Rais wa Marekani ametangaza kuchukua hatua za kuridhisha katika vita vya biashara kati ya Washington na Beijing, akiahirisha kutekelezwa kwa sheria kuhusu ongezeko la kodi mpya kwa dola milioni 250.

Matangazo ya kibiashara

"Hatua hii ni ishara ya nia njema," Donald Trump ameandika katika ukurasa wake wa twitter kabla ya China kusherehekea maadhimisho ya miaka 70.

" Ni ishara ya nia njema," Donald Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwa ombi la Naibu Waziri Mkuu wa China na kiongozi mkuu wa serikali ya Beijing katika mazungumzo na Marekani , Liu He. Hatua hii imechukuliwa kwa hafla maalum: maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China.

Ongezeko hilo jipya la 25% hadi 30% ya kodi kwa bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 250 kutoka China litaahirishwa kwa wiki mbili kati ya Oktoba 1 na Oktoba 15.

Kwa upande wake, China awali ilitangaza kufuta kodi za ziada kwenye aina kumi na sita ya bidhaa kutoka Marekani.

Pamoja na hatua hizi za nia njema katika vita vya biashara kati ya nchi hizi mbili za kwanza zilizostawi kiucumi dunia. viliyodumu miezi 18, vitisho bado vipo.

Mazungumzo kati ya Washington na Beijing yanatarajiwa kuanza tena mapema mwezi Oktoba kwa mara ya kwanza tangu Mei kwa ngazi ya mawaziri.

Ikiwa hakutapatikana mkataba wowote hadi mwishoni mwa mwaka huu, Donald Trump anatarajia kuongeza kodi kwa bidha karibu zote zinazoingia nchini Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.