MAREKANI-TRUMP-ZELENSKIY-SIASA

Ripoti: Ikulu ya ya Marekani yazuia kupatikana kwa mawasiliano ya Trump na viongozi wa nje

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump 路透社

Ripoti za vyombo vya Habari nchini Marekani zinaeleza kuwa Ikulu ya nchi hiyo, imezuia kuonekana au kupatikana kwa mazungumzo kwa njia ya simu ambayo yamekuwa yakifanyika kati ya rais Donald Trump na viongozi wa kigeni.

Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja, baada ya wiki hii kubainika kuwa rais Trump kwa njia ya simu na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alitaka kuchunguzwa kwa aliyekuwa Makamu wa rais Joe Biden.

Biden, anayetafuta tiketi ya chama cha Democratic, anaonekana kuwa mpinzani mkubwa wa kisiasa wa rais Trump kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Inaripotiwa kuwa, sasa ni vigumu kupata taarifa zozote za mazugumzo hasa kati ya rais Trump na rais wa Urusi Vladimir Putin na MwanaMflame wa Saudi Arabia.

Kitendo hicho cha rais Trump kimesababisha wabunge kuanza mchakato wa kuchunguza uwezekano wa kuondolewa kwake madarakani, wakati huu rais Trump kwenye ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa njia ya video, akisema Marekani kwa sasa ipo katika njia panda kwa sababu ya wabunge wa chama cha Democratic.