PERU-SIASA-USALAMA

Peru: Bunge lafutwa, Rais asimamishwa kazi

Waandamanaji wakiomba Bunge kuvunjwa, wakimuunga mkono Rais Martin Vizcarra, Lima, Septemba 30.
Waandamanaji wakiomba Bunge kuvunjwa, wakimuunga mkono Rais Martin Vizcarra, Lima, Septemba 30. Cris Bouroncle / AFP

Mvutano unaendelea nchini Peru kati ya Rais Martin Vizcarra na Baraza la wawakilishi, linaloongozwa kwa idadi kubwa na upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Wabunge walichukuwa hatua ya kufuta ombi la rais la kuahirisha Uchaguzi Mkuu kwa mwaka mmoja ili kuzuia uendeshwaji kazi wa taasisi za nchi. Jumanne hii, Oktoba 1, Rais amejibu kwa kutangaza Bunge kufutwa.

Huenda ikawa ndio mwisho wa mvutano wa muda mrefu kati ya Rais Martin Vizcarra na Baraza la wawakilishi, unaotawaliwa na upinzani. Siku ya Jumatatu jioni, Septemba 30, wakati wabunge walikuwa wakijiandaa kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais, Rais Martin Vizcarra aliamua kuvunja Bunge na kuitisha uchaguzi mpya wa wabunge. Kutokana na hatua hiyo, rais huyo amesimamishwa kwenye wadhifa wake na wabunge.

Sintofahamu ya kisiasa inaendelea nchini Peru, siku moja baada Rais Martin Vizcarra, kuchukuwa hatua ya kuvunja Bunge, huku wabunge kwa upande mwingine wakichukuwa uamuzi wa kumsimamisha kazi rais wao kwa muda wa mwaka mmoja na kuteua rais wa mpito.

Katika hotuba ya televisheni kwa taifa, Bwana Vizcarra alianza kwa kutangaza kufutwa kwa Bunge, ikiwa ni tukio la kwanza kutokea nchini Peru tangu mwaka 1992, na kuitishwa kwa uchaguzi wa wabunge wa mapema Januari 26 mwakani.

Baadhi ya wananchi wa Peru walimiminika mitaani kwa kushangilia hatua hiyo ya rais ya kuvunja Bunge.

Wengi wamsema hatu hiyo inaonyesha kuimarika kwa demokrasia nchini Peru na wanaamni kwamba sasa rushwa itakomeshwa.

Kwa wiki kadhaa wananchi wa Peru wameendelea kuandamana wakiomba rushwa ikomeshwe nchini humo, wakiwashtumu wabunge ambao wengi ni kutoka upinzani kujihusisha na rushwa.