Pata taarifa kuu
VENEZUELA-UN-HAKI

Venezuela yapingwa kuwania kiti kwenye Baraza la Haki za Binadamu

Wajumbe wakishiriki katika ufunguzi wa kikao cha 42 cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Septemba 9, 2019.
Wajumbe wakishiriki katika ufunguzi wa kikao cha 42 cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Septemba 9, 2019. © AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa umeitishwa leo Alhamisi kuchagua wajumbe wapya 14 wa Baraza la Haki za Binadamu, moja ya nafasi ambazo Venezuela inatarajiwa kuchikilia licha ya upinzani kutokamashiriki yasio ya kiserikali na nchi za Amerika ya Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Haki za Binadamu, lenye makao yake makuu mjini Geneva, nchini Uswisi, lina jukumu la kuimarisha ukuaji na kulinda haki za binadamu. Wajumbe wake 47 wanachaguliwa kila mwaka kwa karibu theluthi moja kati yao. Nafasi hizo hujazwa tangu mwezi Januari kwa muda wa miaka mitatu na kura imepangwa kufanyika kuanzia saa nane saa za kimataifa (sawa na kumi saa za Afrika ya Kati).

Uundwaji wa baraza hilo la Haki za Binadamu, ambalo liliundwa mnamo mwaka 2006, unaheshimu kanuni ya idadi kwa kila bara, ikiwa ni sawa na viti 13 kwa Afrika, viti 13 kwa ukanda wa Asia na Pacific, viti 8 kwa Amerika ya Kusini na Karibiani, viti 7 kwa Ulaya Magharibi na nchi zingine. Na viti 6 kwa Ulaya ya Mashariki.

Mwaka huu, uwakilishi wa Venezuela, nchi inayoendelea kukumbwa na mgogoro, unakabiliwa na utata mkubwa. Nchi zaidi ya hamsini zinamchukulia rais Nicolas Maduro kuwa si rais halali wa nchi hiyo na kumuunga mkono mpinzani wake Juan Guaido. Amerika ya Kusini inatarajiwa kupata viti viwili. Brazil inawania kiti kimoja na Oktoba 3 Costa Rica iliomba kuwania kiti kinachosalia kwa kuiangusha Venezuela.

"Kwa sababu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu" ulioshuhudiwa na Umoja wa Mataifa, "serikali ya Venezuela haiwezi kuwania nafasi kwenye Baraza la Haki za Binadamu", alieleza wakati huo Rais wa Costa Rica , Carlos Alvarado.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.