MAREKANI-MAJANGA ASILIA

Marekani: Califorinia yaendelea kukumbwa na mikasa mikubwa miwili ya moto

Helikopta ikiruka juu ya eneo linalokumbwa na moto unaothiri magharibi mwa Los Angeles, Oktoba 28, 2019.
Helikopta ikiruka juu ya eneo linalokumbwa na moto unaothiri magharibi mwa Los Angeles, Oktoba 28, 2019. REUTERS/Gene Blevins

Mikasa miwili mikubwa ya moto inaendeea kuliandama Jimbo la California, hasa Kaskazini mwa jimbo hilo na Jimbo la Los Angeles, huku wakaazi wa meneo mbalimbali ya majimbo hayo wakihamishwa kila siku.

Matangazo ya kibiashara

Moto umeshika kasi katika eneo la Sonoma, Kaskazini mwa California katika saa zisizozidi 24.

Moto huo tayari umeshaharibu heka 26,000 za msitu. Karibu watu 180,000 walitakiwa kuhama makaazi yao mwishoni mwa wiki hii iliyopita kutokana na moto huo unaojulikana kwa jina la "Kincade Fire", kaskazini mwa San Francisco. Maafisa 3,400 wa Zima Moto wametumwa tangu Jumatano iliyopita katika maeneo mbalimbali yanayokumbwa na mikasa hiyo ya moto.

Watu wengi wanahofia kuzuka kwa moto mkali kama ule uliozuka katika jimbo hilo miaka miwili iliyopita, na kuuwa watu 44. Mamlaka imeendelea kutoa wito kwa wakaazi wa maeneo hayo kuhama haraka na kutoweka hatarini maisha yao.