Pata taarifa kuu
BOLIVIA-SIASA

Bolivia: Evo Morales atangaza kwenda Mexico na kuahidi kurudi na "nguvu zaidi"

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa  Mexico, Evo Morales mwenyewe aliomba hifadhi ya kisiasa nchini Mexico.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico, Evo Morales mwenyewe aliomba hifadhi ya kisiasa nchini Mexico. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Rais wa Bolivia aliyeshinikizwa kujiuzulu kufuatia maandamano makubwa yaliyokuwa yakiendelea nchini humo, Evo Morales, ametangaza katika ujumbe kuondoka nchini Bolivia na kwenda Mexico.

Matangazo ya kibiashara

Bw Morales amekaribisha serikali ya Mexico iliyokubali kumpa hifadhi ya kisiasa.

Ameahidi kurudi na "nguvu nyingi na uwezo zaidi".

"Inaumiza kuondoka nchini kwa sababu za kisiasa, lakini bado niko katika hali ya kusubiri. Hivi karibuni, nitarudi na nguvu nyingi na uwezo zaidi, "ameandika rais huyo wa zamani kwenye akaunti yake ya Twitter.

Evo Morales aliamua kuachia ngazi kwenye uongozi wa nchi, baada ya wiki tatu za maandamano makubwa dhidi ya kuchaguliwa kwake tena kwa muhula wa nne. Hatua hiyo ilikuja wakati jeshi na polisi walikuwa wamemtaka aondoke madarakani.

"Ninaachia nafasi yangu kama rais," kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 60, ambaye amekuwa madarakani tangu 2006, alisema kwenye runinga ya taifa Jumapili Novemba 10.

Marais wa Cuba na Venezuela wamesema Evo Morales amelazimika kuachia ngazi kufautia shinikizo la baadhi ya nchi za kimagharibi ambazo zimeshinikiza jshi kufanya mapinduzi dhidi ya utawala wa Evo Morales.

Saa moja kabla ya hatua ya Evo Morales ya kujiuzulu, Mkuu wa majeshi ya Bolivia, Vladimir Yuri Calderon, alikuwa amemtaka rais huyo kung'atuka madarakani.

Kamanda wa jeshi nchini humo, amewataka wanajeshi kuungana na polisi kusaidia kutuliza ghasia ambazo zimeongezeka baada ya Morales kuamua kuondoka madarakani.

Wafuasi wake wamepambana na polisi na zaidi ya watu 20 wamejeruhiwa.

Naibu kiongozi wa bunge la Senate anatarajiwa kuwa rais wa mpito hadi pale uchaguzi mwingine utakapofanyika.

Morales alichagua mara ya kwanza mwaka 2006, na katika uongizi wake atakumbukwa kupambana na umasikini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.