Pata taarifa kuu
MAREKANI-CARTER-AFYA

Jimmy Carter alazwa hospitalini baada ya kuanguka

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter (kushoto), Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan (katikati) na Graca Machel (kulia), mke wa Nelson Mandela, katika mkutano na waandishi wa habari Novemba 22, 2008 Johannesburg.
Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter (kushoto), Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan (katikati) na Graca Machel (kulia), mke wa Nelson Mandela, katika mkutano na waandishi wa habari Novemba 22, 2008 Johannesburg. (Photo : AFP)
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter amelazwa hospitalini Jumatatu wiki hii ili kufanyiwa matibabu kichwani baada ya kuanguka hivi karibuni, Wakfu uliopewa jina lake umetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Jimmy Carter "alilazwa katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory Jumatatu wiki hii alasiri katika kufanyiwa matibabu kwa kupunguza shinikizo kwenye ubongo wake, lililosababishwa na kutokwa na damu baada ya kuanguka hivi karibuni," kilisema chanzo hicho na kuongeza kuwa upasuaji huo umepangwa Jumanne hii asubuhi.

"Rais Carter anaendelea vizuri na mkewe Rosalynn yuko naye," kimeongeza chanzo hicho.

Jimmy Carter alilazwa hospitalini mwishoni mwa mwezi Oktoba baada ya kupata jeraha kwenye nyonga alipoanguka nyumbani kwake. Wakfu wake ulieleza kwamba jeraha "halihatarishi maisha yake".

Jimmy Carter, ambaye ni rais wa kwanza wa Marekani katika historia kufikia umri wa miaka 95, pia alijeruhiwa kichwani Oktoba 6, alipoanguka nyumbani kwake.

Jimmy Carter, rais wa zamani aliyechaguliwa kidemokrasia (1977-1981) hata hivyo alikuwa vizuri kiafya siku mbili zilizopita, licha ya kuwa alikuwa bado akiuguza majeraha madogo aliyoyapata mwezi uliyopita.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.