Pata taarifa kuu
BOLIVIA-SIASA-USALAMA

Seneta Jeanine Añez ajitangaza kuwa rais wa mpito Bolivia

Seneta wa upinzani Jeanine Añez, ambaye amejitangaza kuwa rais wa mpito wa Bolivia.
Seneta wa upinzani Jeanine Añez, ambaye amejitangaza kuwa rais wa mpito wa Bolivia. REUTERS/Manuel Claure
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Makamu wa Pili wa Rais wa Bunge la Seneti nchini Bolivia, Jeanine Añez, amejitangaza kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo, siku chache tu baada ya Evo Morales kulazimika kuachia ngazi.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Evo Morales anayeendelea kudai kuwa alipinduliwa kimabavu, amesema anataka kuendelea na "mapambano" atakapowasili Mexico.

Makamu wa pili wa Rais wa Seneti Jeanine Añez amejitangaza kuwa rais wa mpito wa Bolivia, licha ya kukosekana kwa idadi ya wabunge inayohitajika, akisema ameamua hivo kutokana na kwamba kuna " umuhimu wa kuweka mazingira sawa ya amani ya kijamii" katika nchi hii inayoendelea kukumbwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa.

"Tunataka kuitisha uchaguzi haraka iwezekanavyo," ameongeza seneta huyo wa upinzani ambaye anadai kuwa ni urais wa mpito baada ya kujiuzulu kwenye nyadhifa zao Evo Morales, Makamu wa rais Alvaro Garcia Linera, rais na makamu wa rais wa Bunge la Seneti na pia Spika wa Baraza la wawakilishi.

Evo Morales ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema tangazo hilo la Seneta Añez ni "jaribio la mapinduzi".

"Jaribio la mapinduzi la kushangaza na la aibu katika historia ya Bolivia limefanyika. Seneta kutoka mrengo wa kulia uliofanya jaribio la mapinduzi amejitangaza kuwa rais wa Seneti, kisha kaimu rais wa Bolivia bila idadi inayohitajika ya wabunge kupasisha tangazo lake, huku akizungukwa na kundi lililohusika katika jaribio hilo la mapinduzi na kuongozwa na jeshi na polisi wanaokandamiza raia. " Bw Morales ameandika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.