Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Ushuhuda wa kwanza: Rais Trump alitaka Biden afanyiwe uchunguzi

Wanadiplomasia wawaili wa ngazi ya juu William Taylor (kulia) na George Kent mbele ya Baraza la Congress la Marekani, Novemba 13, 2019.
Wanadiplomasia wawaili wa ngazi ya juu William Taylor (kulia) na George Kent mbele ya Baraza la Congress la Marekani, Novemba 13, 2019. REUTERS/Erin Scott
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Mahojiano ya kwanza ya hadhara yameanza katika Bunge la Marekani ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ung'atuzi unaomlernga rais wa nchi hiyo Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Wanadiplomasia wawili wa ngazi ya juu wameonyesha shinikizo lililotolewa kwa Ukraine.

Mahojiano haya ya ung'atuzi dhidi ya Donald Trump yamerushwa moja kwa moja kwenye televiseni. mashuhuda wa kwanza walioanza kusikilizwa na Bunge la Marekani, ni wanadiplomasia wawili wa ngazi ya juu, William Taylor na George Kent ambao wamebaini kwamba Ukraine ilishinikizwa kutoa taarifa ambazo zinaweza kusaidia rais Donald Trump katika kampeni yake anachaguliwa tena.

William Taylor, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu katika ubalozi wa Marekani mjini Kiev, ameripoti kuhusu kikao cha mazungumzo ambacho mmoja wa wasaidizi wake alihudhuria Julai 26 mwaka huu kati ya balozi wa Marekani Gordon Sondland na Donald Trump.

"Msaidizi wangu aliweza kumsikia rais kwenye simu akiuliza maswali Sondland kuhusu uchunguzi. Balozi Sondland alimweleza rais kwamba Ukraine iko tayari kufanyia kazi ombi lake. Baada ya simu hiyo, msaidizi wangu alimuuliza Gordon Sondland kile rais anafikiria kuhusu Ukraine. Balozi Sondland alijibu kwamba Rais Trump anataka Biden afanyiwe uchunguzi. Baada ya hapo sikurudi tena kujuwa kinachoendelea kuhusu mazungumzo hayo. "

Matumizi mabaya ya madaraka

"Siku moja kabla, rais wa Marekani alimuomba mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy "kumchunguza kwa makini" Joe Biden, ambaye atapeperusha bendera ya chama cha Democratic dhidi ya Donald rump katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.

Wabunge kutoka Chama cha Democratic walio wengi waliamua kuanzisha uchunguzi kwa mchakato wa ung'atuzi dhidi ya Dnald Trump baada ya kufichuliwa kwa mazungumzo haya, katikati mwa mwezi Septemba. Wademocrats wanamshtumu Donald Trump kutumia vibaya madaraka yake kwa maslahi yake binafsi, kwa kutoa masharti kwa Ukraine kuweza kupewa msaada wa kijeshi na kukubaliwa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kukubaliwa kupokelewa katika ikulu ya White House ikiwa Ukraine itaanzisha uchunguzi dhidi ya Joe Biden.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.