Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAUAJI-USALAMA

Marekani yaomboleza vifo vya wanafunzi wawili waliouawa Los Angeles

Wanafunzi wa shule ya upili wakishindikzwa na polisi baada ya kuondolewa kutoka shule ya Santa Clarita Novemba 14, 2019.
Wanafunzi wa shule ya upili wakishindikzwa na polisi baada ya kuondolewa kutoka shule ya Santa Clarita Novemba 14, 2019. KHTS Radio via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Vijana wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine watatu wamejeruhiwa, wakati mmoja wao alifyatuwa risasi katika uwanja wa michezo wa shule ya upili ya Santa Clarita, California, nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea Alhmisi Novemba 14. Hii si mara ya kwanza tukio kama hilo kutokea katika shule nchini Marekani. Wanafunzi wengi wamepoteza maisha katika tukio kama hilo.

Mshambuliaji, mwenye umri wa miaka kumi na sita, alichagua siku ya kuzaliwa kwake kuweza kufanya uhalifu huo dhidi ya wenzi wake.

Mshambuliaji huyo aliachia risasi moja katika bunduki yake ili aweze kujimalizia maisha, lakini hakufikia hatua hiyo, baada ya kujipiga risasi na kujeruhiwa, polisi imesema katika mkutano na waandishi wa habari. Mshambuliaji amelazwa hospitalini akiwa katika hali mbaya, polisi imeongeza.

Mwaka uliopita Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba kuwapatia walimu silaha kunaweza kuzuia mashambulio ya risasi katika shule.

Kauli aliitoa baada ya mtu aliyehihami kwa bunduki kuua watu 17 mjini Florida mwaka 2018.

Lakini Mark Barden ambaye mwanawe aliuawa katika shambulio la 2012 katika shule ya Sandy Hook Elementary School mjini Connecticut - anasema ''ongezeko la bunduki sio suluhu. Walimu wana majukumu zaidi kwa sasa kwa wao kuchukua jukumu jingine la kutumia nguvu ili kumuua mtu'', alisema

Majimbo kadhaa ya Marekani tayari yanaruhusu bunduki ndani ya vyuo na taasisi za elimu kulingana na tovuti ya kujihami katika vyuo. Jimbo la Florida hatahivyo halifanyi hivyo.

Tangu mwanzoni mwa mwaka, wanafunzi hawa wawili wametimiza idadi ya watu 366 ambao wameuawa kwa kupigwa risasi nchini Marekani, kwa mujibu wa tovuti Gun violence Archive.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.