Pata taarifa kuu
BOLIVIA-SIASA-USALAMA

Bolivia: Utawala wa mpito waahidi kuitisha uchaguzi 'haraka sana'

Kaimu Rais wa Bolivia Jeanine Añez katika mkutano na waandishi wa habari, La Paz Novemba 15, 2019.
Kaimu Rais wa Bolivia Jeanine Añez katika mkutano na waandishi wa habari, La Paz Novemba 15, 2019. RONALDO SCHEMIDT / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kaimu rais wa Bolivia, Jeanine Añez, ametangaza kwamba utawala wake unatarajia kuitisha uchaguzi "wa wazi" haraka sana ", wakati hali inaendelea kuwa mbaya zaidi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Tayari pande mbili katika mgogoro nchini Bolivia zimeanza kushtumia kwa kile baadhi wanasema uhalifu dhidi ya binadamu unaendelea.

Hata hivyo utawala uliopo madarakani sasa unasema kuwa hali imeanza kuwa shwari, lakini Evo Morales, arai aliyelazimika kuachia madaraka na kukimbilia nchini Mexico anaishtumua serikali kutekeleza "uhalifu dhidi ya binadamu".

"Hivi karibuni tutatoa taarifa kuhusu jukumu letu kuu: kuitishwa kwa uchaguzi wa wazi," Añez amesema katika hotuba yake alioitoa kwenye makao makuu ya serikali mjini La Paz.

Hakutoa maelezo zaidi, lakini amesema tangazo lijalo litakuwa na lengo la kutafuta "kurudisha uaminifu wa demokrasia kwa nchi yetu".

Jeanine Añez, mbunge kutoka mrengo wa kulia mwenye umri wa miaka 52, anashikilia wadhifa wa rais tangu Jumanne wiki iliyopita kama spika wa pili wa rais wa Bunge la Seneti, wakati viongozi wa juu wa taasii hiyo ambao wangelichukuwa nafasi hiyo kulingana na katiba ya nchi walijiuzulu kwenye nyadhifa zao.

Evo Morales, ambaye alikuwa rais tangu mwaka 2006, alijiuzulu Jumapili ya wiki iliyopita, baada ya kupoteza imani kwa jeshi, na kukimbilia uhamishoni nchini Mexico.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.