Pata taarifa kuu
CHILE-SIASA-USALAMA

Chile: Rais wa Chile alaani vurugu za polisi

Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi Novemba 16, 2019 Santiago, Chile.
Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi Novemba 16, 2019 Santiago, Chile. © AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa maandamano ya kiraia mwezi uliopita nchini Chile, Rais Sebastian Piñera amelaani vurugu zilizosababishwa na polisi dhidi ya waandamanaji.

Matangazo ya kibiashara

"Kulikuwa na matumizi ya nguvu, dhulma au makosa yalifanywa na haki za wote hazikuheshimiwa," rais Piñera amekiri katika htuba iliyorushwa kwenye televisheni kutoka ikulu ya rais ya La Moneda Jumapili Novemba 17.

Mgogoro huo ambao unaendelea kuikumba nchi hii ya Amerika Kusini tangu Oktoba 18 umeuwa watu 22, wengi wao katika mikasa ya moto wakati wa uporaji na watano kutokana na matumizi ya nguvu ya vikosi vya usalama, na zaidi ya watu 2000 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa shirika la kitaifa la Haki za Binadamu (INDH), shirika huru la umma, karibu watu 200 wamepigwa risasi za mpira kwenye jicho wakati polisi ilikuwa ikijaribu kutawanya waandamanaji.

Rais wa Chile amehakikishia kuwa hakutakuwa na "adhabu yoyote", "kwa wale ambao walifanya vitendo vya ukatili," akimaanisha uharibifu na uporaji uliotekelezwa na waandamanaji wenye msimamo mkali, " pamoja na wale ambao wamefanya dhulma (...) na uhalifu mwengine, " akimaanisha polisi na wanajeshi.

"Tutafanya kilio chini ya uwezo wetu kuwasaidia waathiriwa," amesema piñera, ambaye pia ametoa rambirambi zake kwa familia zilizopoteza ndugu zao.

Vitendo vya udhalilishaji, unyanyasaji wa kijinsia, mateso,...: mashtaka na malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na maafisa wa polisi yameongezeka tangu kuanza kwa maandamano, na kupelekea Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe wa uchunguzi kuhusu uhalifu uliotokea nchini humo.

Siku ya Ijumaa, katika maandamano mapya katika mji wa Santiago, katika eneo la muhimu la Plaza Italia, polisi ilishtumiwa na mashirika kadhaa ya haki za binadamu kwamba walichelewesha zoezi la kumsafirisha kijana mmoja hospitali aliyepatwa na mshtuko wa moyo, baada ya kurusha gesi ya machozi dhidi ya wauguzi.

Sebastian Piñera pia amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa siku ya Ijumaa na vyama vya siasa kuhudu kufanyika kwa kura ya maoni mwezi Aprili 2020 ili kubadilisha Katiba ya sasa, iliyowekwa tangu wakati wa utawala wa kiimla wa Augusto Pinochet (1973-1990) na inashtumiwa kuwatenga baadhi ya watu katika jamii.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.