Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Kesi ya ung'atuzi dhidi ya Trump: Mahojiano ya hadhara kuanza tena

Donald Trump wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Oktoba 9, 2019.
Donald Trump wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Oktoba 9, 2019. REUTERS/Jonathan Ernst
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Baraza la Wawakilishi la Marekani linaanza Jumanne wiki hii mfululizo wa mahojiano ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ung'atuzi unaomlernga rais wa nchi hiyo Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Mashahidi tisa wanatarajiwa kusikilizwa kwa muda wa zaidi ya siku tatu, ikiwa ni pamoja na balozi ambaye anawavutiwa sana Wademocrats.

Washauri wa Ikulu ya White, wanadiplomasia na maafisa wakuu wa utawala wa Trump wataandamana mbele ya Kamati ya upelelezi ya Baraza la Wawakilishi, ambayo inaongoza uchunguzi dhidi ya rais wa Marekani.

Ushuhuda wao utatangazwa moja kwa moja kwenye runinga, kama ule wa wanadiplomasia watatu waliosikilizwa wiki iliyopita.

Mashuhuda wa kwanza walioanza kusikilizwa na Bunge la Marekani, ni wanadiplomasia wawili wa ngazi ya juu, William Taylor na George Kent ambao walibaini kwamba Ukraine ilishinikizwa kutoa taarifa ambazo zinaweza kusaidia rais Donald Trump katika kampeni yake anachaguliwa tena.

William Taylor, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu katika ubalozi wa Marekani mjini Kiev, aliripoti kuhusu kikao cha mazungumzo ambacho mmoja wa wasaidizi wake alihudhuria Julai 26 mwaka huu kati ya balozi wa Marekani Gordon Sondland na Donald Trump.

Picha za mashahidi wanane ambao watasikilizwa wiki hii katika Bunge la Marekani, katikati mbenge kutoka chama cha Democratic Adam Schiff anayesimamia uchunguzi kuhusu kesi ya ung'atuzi dhidi ya Donald Trump.
Picha za mashahidi wanane ambao watasikilizwa wiki hii katika Bunge la Marekani, katikati mbenge kutoka chama cha Democratic Adam Schiff anayesimamia uchunguzi kuhusu kesi ya ung'atuzi dhidi ya Donald Trump. © AFP
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.